DAMU YA YESU
Damu ya Yesu ni Damu ya Mungu aliyejifanya mwanadamu
kwa ajili ya kuja kumkomboa mwanadamu katika dhambi .Kwa hiyo Damu yake
ilifanya kazi ya kuondoa sauti ya shetani ndani ya damu ya mwanadamu iliyokuwa
imechafuliwa na shetani na kurudisha sauti ya Mungu kama ilivyokuwa awali kabla
ya Anguko la Adamu na Hawa pia na
kutengua maagano yote yaliyokuwa yamefanywa na wanadamu kwa njia ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu
wakitumia damu za wanyama na
kuwarudisha katika mstari na hali ya
kuwa na maagano mazuri na Mungu wa Ibrahimu ,Isaka na Yakobo kupitia hiyo Damu.
Damu ya Yesu ni Damu ya thamani kuliko damu ya mnyama
au mwanadamu yoyote maana haina ila wala waa kama tunavyosoma katioka kitabu
cha 1 Petro 1:19 Bali mlikombolewa
kwa Damu ya thamani ,kama ya mwanakondoo asiye na ila na waa ,yaani Kristo
Kwa sababu ya Utakatifu wake Damu ya Yesu inanena mema
kwa ajili ya maisha ya mwanadamu kwa ujumla wake maana inalenga kumkomboa
mwanadamu kutoka katika gereza la dhambi na kuonewa na shetani.Damu hii
inaneana mema kwa ajili ya Afya,Ndoa ,Shughuli ,Uzao,Huduma,Mipango na kila
kitu kilicho chema cha mwanadamu ili aweze kufanikiwa bila usumbufu wowote wa
ibilisi.
Damu ya Yesu ikikunenea mema hakuna awezaye kutengua
Ebrania 12:24 na Yesu mjumbe wa agano jipya,na damu ya
kunyunyizwa,inaneyo mema kuliko ile ya habili
Yohana 19:34 na mara ikatoka Damu na maji
1 yohana 5: 8-9 kwa maana wako watatu washuhudiao (mbinguni,Baba na
Neno ,na Roho Mtakatifu na watatu hawa ni umoja).Kisha wako watatu washuhudiao
duniani Roho,na maji na Damu na
watatu hawa kupatana kwa habari
moja.Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu ,ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi
kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu ,kwamba amemshuhudia Mwanawe.
Kwa hiyo tuanaona kwamba Damu ya Yesu inashuhudia yanayotendeka duniani kwa
maana kwamba yote tuyatendayo Damu ya Yesu inayaona na kutoa ripoti mbinguni
kwa Baba.
KAZI YA DAMU YA YESU
1.
Inanena mema
Ebrania 12:24/1 Petro 1:2
2.
Damu ya Agano
Ebrania 9:20 1Korintho 11:25-29 kutoka 24:6-8(Musa),Mathayo 26:28/27:24
3.
Hutusafisha
makosa 1 Yohana 1:7/ufunuo 19:13/ufunuo 5:9/Ebrania 9:24
4.
Tunapata ushindi
Ufunuo 12:11
5.
Amani tunapata
Kolosai 1:20
6.
Husafisha dhamiri
zetu Ebrania 9:24
7.
Kuhesabiwa haki
Rumi 5:9
8.
Upatanisho Rumi
3:25
9.
Ondoleo la dhambi
Ebrania 9:22/Ufunuo 1:5
10. Hututakasa sisi Ebrania 13:12
11. Hutuleta karibu na Mungu Kolosai 1:20-21
12. Hutupa ujasiri wa kuingia kwenye uwepo wa Mungu
Ebrania 10:19-22
13. Hutukamilisha machoni pa Mungu Ebrania 10:14
MLINGANISHO BAINA YA DAMU YA MNYAMA, DAMU YA
MWANADAMU NA DAMU YA YESU
DAMU YA WANYAMA
|
DAMU YA
MWANADAMU
|
DAMU YA YESU
|
Haina uhai wa Mungu
|
Ina uhai wa Mungu
|
Ina uhai wa Mungu
|
Mnyama anapokuwa mdogo damu yake haina mawaa
lakini inapokuwa kubwa ina mawaa.
|
Ina mawaa
|
Ni safi ,Haina mawaa,ni Takatifu
|
Haiwezi kuondoa dhambi
|
Haiwezi kuondoa dhambi
|
Inaondoa na kutakasa dhambi
|
Inatengeneza
Agano na Ibilisi baada ya Ukombozi kwa Damu ya Yesu
|
Kwa njia ya kutolewa Kafara za watu inatengeneza agano na Ibilisi .
|
Inatengeneza
Agano na Mungu
|
Shetani anaitumia kufanya maagano na wanadamu
|
Shetani huitumia kufanya maagano na wanadamu
|
Mungu wa Ibrahimu ,Isaka na Yakobo anaitumia kufanya
maagano na wanadamu
|
Hutuleta karibu na shetani iwapo tutaitumia
kufanya maagano au kwa manuizo.
|
Hutuunganisha na wanadamu wengine katika
tendo la Ndoa.
Hutuunganisha na ibilisi endapo tunatoa
kafara za watu.
|
Hutuleta karibu na Mungu
|
ANGALISHO:
Ibada yoyote inayofanyika kwa kutumia damu tofauti na Damu ya Yesu na
Jina tofauti na Jina la Yesu Kristo hiyo ni ibada ya miungu .
Kuanzia ujio wa Yesu Hakuna aina ya damu yoyote inayoweza kutumika
kufanya agano na Mungu aliye hai.
AHADI KUHUSU DAMU:
1.
Yoeli 3:21 nitaitakasa damu ambayo sijaitakasa
2.
Yohana 6:53-54
3.
Ezekiel 16:6-9
DALILI YA NAFSI ILIYOFUNGWA HAIJAKOMBOLEWA KUTOKANA
NA MAAGANO YA DAMU
- Mtu hushindwa
kujitawala(mtu anashindwa kuweka mambo ya nyumba yake vizuri)
- Mtu mwenye matatizo
yanayojirudia-rudia(mf magonjwa,kupoteza fedha…)
- Hali ya kutokuendelea
katika maisha
- Anaishi maisha ya kuanza
–anza na kushindwa-shindwa
- Kutojiamlia mambo yako
mwenyewe(akili yako imepumbazwa).Maisha ya kutegemea kuambiwa ambiwa.
- Dalili ya kutumia nyuvu
nyingi lakini matokeo madogo(mwanzo4:11)(kulima,kazi,biashara)kuishi
maisha ya kukata tamaa
naishuhudia mbingu na nchi(ardhi) hushirikiana kutambua (laana na
Baraka ) ardhi na mbingu hushirikiana katika kutoa mvua,kuzalisha …..
- Kurithi matatizo ya wazazi
,ya ukoo Ezekiel 16:44 alivyo mama ndivyo alivyo binti yake,alivyo baba
ndivyo alivyo mtoto wa kiume.
- Ndoto mbaya-mbaya
- Kukosa ulichostahili kuwa
nacho
- Kudharauliwa na watu
waliostahili kukuheshimu(zaburi 113:7)
- Kuishi katika uhitaji wa
kukithiri(ufukara)
- Kuishi bila mafanikio
kifedha (hagai 2:8)
- Utasa wa
kibinadamu,wanyama,ardhi,biashara
- Kuishi bila kazi,shuguli
yoyote,kuwa ombaomba
- Kuishi katika mikosi na
balaa(hasara juu ya hasara)
- Kuishi katika dhambi
isiyoisha inayokufadhehesha Methali 28:13
MWALIMU JAMES SADY 0717 820 980
E-MAIL:jamesady9@gmail.com